Idara ya huduma za polisi nchini imeomba madereva kote nchini kuwa wastaarabu na waangalifu wanapotekeleza majukumu yao, ili kuepuka ajali za barabara, hasa wakati huu wa shamrashamra.

Wito huu unafuatia ajali mbaya ya barabara kushuhudiwa asubuhi ya leo katika eneo la Governor kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu kuelekea Naivasha. Ajali hiyo ilihusisha lori mbili ambazo ziligongana ana kwa ana na kuwaka moto papo hapo.

Taarifa kutoka kwa idara za usalama zimebaini kuwa maafisa wa polisi kutoka katika kituo cha Mai mahiu walisaidia kukabiliana na moto huo, huku majeruhi wakipelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha ambapo wanaendelea kupokea matibabu.

December 14, 2022