Zoezi la kuwachanja mifugo katika kaunti ya Narok limeng’oa nanga hii leo baada ya idara ya kilimo na mifugo kupokea dozi 510,000 za chanjo ya mifugo.

Akizungumza baada ya kupokea dozi hizo, waziri wa kilimo Joyce Keshe amesema kuwa zoezi hilo limeanza katika maeneo ya Nturumeti, Mosiro na Ongata Naado, Narok mashariki.

Wakulima wametakiwa kupeleka mifugo wao katika maeneo ambayo wataelekezwa na machifu. Kando na hayo, Bi. Keshe amemshuruku gavana wa kaunti hii Patrick Ntutu kwa kufadhili ununuzi wa dozi hizo.

Mbali na serikali ya Narok, taasisi ya kilimo na chakula FAO kwa ushirikiano na shirika la UN vilevile zilichangia ununuzi wa dozi hizo.

December 15, 2022