Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameongoza hafla ya uzinduzi wa safari ya ndege ya kwanza kabisa kuelekea katika kaunti ya Kakamega.

Hafla ya uzinduzi wa safari hiyo iliandaliwa katika uwanja wa ndege wa Wilson Jijini Nairobi, na kushuhudia ndege ya abiria ya kampuni ya Skyward Express ikianza safari hiyo kuelekea katika kaunti ya Kakamega, kuashiria mwanzo wa safari za ngege kuelekea katika kaunti hiyo ya magharibi.

Gachagua aliyeandamana na viongozi wa serikali akiwemo Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema kuwa hatua hiyo itafungua sekta ya utalii wa ndani sawa na kubuni nafasi za ajira kwa watu wa magharibi.

December 14, 2022