Mahakama kuu imeongeza muda wa amri ya kuwazuia polisi kumhoji wakili Danstan Omari kwa madai ya kuvamiwa kwa nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’I.

Mahakama iliamuru kesi hiyo itajwe Aprili 18 kwa mwelekeo zaidi baada ya pande zote kuwasilisha ombi lao na kujibu ombi hilo.Wakati huo huo, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amewasilisha majibu yake akisema kuwa haki ya wakili-mteja haihusu matendo ambayo ni kiasi cha kutenda kosa la jinai.

Zaidi ya hayo, polisi wameiomba mahakama kutotoa amri iliyoombwa na Omari, wakisema watanyimwa jukumu lao la kuchunguza suala hilo.

Katika kesi hiyo, Omari alifikishwa mahakamani akisema haki yake ya kuwa wakili inakiukwa na kuongeza kuwa wito unaotolewa na polisi ni kudhalilisha utendaji wa mawakili kwa kuingilia mawasiliano wanayofanya na mteja.

Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Jaji Hedwig Ongudi ambaye aliagiza chama cha Wanasheria wa Kenya kuwasilisha majibu yao.

March 9, 2023