BY ISAYA BURUGU,31ST JAN 2023- Papa Francis leo anatarajiwa kutua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nyumbani kwa jumuiya kubwa zaidi ya wakatoliki wa Roma barani Afrika, kwa ziara ya siku tatu.

Ni zaidi ya miaka 37 tangu Papa wa zamani , John Paul II, alipoitembelea nchi hiyo – ilipoitwa Zaire.Mamlaka nchini humo imetangaza Jumatano kuwa siku ya mapumziko katika mji mkuu, Kinshasa, ili kuwaruhusu Wakatoliki kuhudhuria misa inayoongozwa na Papa Francis katika uwanja wa ndege wa Ndolo.

Papa Francis ameomba sala kwa ajili ya safari kabla ya kuondoka kwake.Papa atasalia Kinshasa hadi Ijumaa kabla ya kusafiri hadi mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, ambako ataungana na mwenzake wa Anglikan, Askofu Mkuu wa Canterbury na Moderator wa Kanisa la Scotland.

Hata hivyo, kumekuwa na utata kuhusu ziara ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki mjini Kinshasa.

Baadhi ya wafanyakazi wa soko hilo mjini humo wametakiwa kuvunja vibanda vyao ili kutengeneza barabara kabla ya papa kuwasili.Hili limewaacha baadhi ya watu kuhisi huzuni.

 

 

 

 

January 31, 2023