BY ISAYA BURUGU,31ST JAN,2023-Washukiwa watatu wa wizi wakimabavu  wamekamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya maafisa wa polisi  kuwapata na bidhaa za kielktroniki zilizoibiwa katika mtaa wa Githurai 44 kaunti ya Nairobi.Washukiwa hao,Francis Itaru, Joel Njoroge na  John Warui walikamatwa baada ya maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kasarani  kupashwa Habari.

Taarifa kutoka idara ya upelelezi wa jinai DCI  aidha imeongeza kuwa  maafisa wa polisi walikuwa wamefahamishwa kuhusu magari mawili ambayo yamekuwa yakibeba bidhaa za kielektroniki  ambazo baadaye huuziwa wafanyibiashara katika eneo hilo.

Washukiwa/Picha/Hisani

 

Watatu hao wamepatikana wakiwauzia  wachuuzi bidhaa za kielektroniki  na msako wa haraka ukaendeshwa  katika gari lao ambapo nambari bandia za usajili  wa magari ,funguo kadhaa,kipakatalishi  na vifaa vya kuvunja nyumba vilipatikana.

Kwa sasa washukiwa hao wanazuiliwa  katika kituo cha polisi cha Kasarani wakisubiri kufikishwa mahakamani.

 

 

 

 

January 31, 2023