Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu tawi la Narok hii leo wamewatembelea waathiriwa wa mkasa wa moto uliotukia katika eneo la mong’are majuma matatu yaliyopita.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi waathiriwa hao msaada wa bidhaa kama vile vyombo na blanketi, mratibu wa shirika hilo Celestine Oguto amesema mkasa huo ulisababisha maafa makubwa kwa wakaazi hao ikizingatiwa kwamba wengi wamekosa makao na chakula. Ameongeza kuwa shirika hilo litashirikiana na wakaazi wa Narok ili kuweka mikakati itakayowasaidia waka wa majanga.

Kwa upande wao, wakaazi  hao wamelishukuru shirika hilo kwani walikuwa wamepoteza kila kitu kutokana na mkasa huo.

January 31, 2023