BY ISAYA BURUGU,8TH MARCH 2023– Maafisa wa polisi  wanachunguza  kifo cha kutatanisha cha  mrembeshaji nyumba  Geoffrey Mwathi, aliyefariki baada ya kuanguka  kutoka kwa orofa ya kumi ya jumba la  Redwood kwa njia isiyojulikana.

Mwathi,mwenye umri wa  23, anasemekana  kufariki baada ya kuanguka  kutoka kwa dirisha la nyumba  ya kukodi ya  mwanamuziki maarufu wa benga wa nyimbo za agikuyu  DJ Fatxo,amabye jina lake hasli ni Lawrence Njuguna.

Kwa mjibu wa ripoti marehemu Mwathi alikomboewa na DJ  kurembesha  vyumba viwili vya nyumba yake Afisi na Duka.Marehemu anasemekana kuondoka nyumbani kwake tarehe 21 mwezi jana   kukutana na Dj  na kutamatisha mikakati ya kazi.

Marehemu Jeff Mwathi/Picha -Hisani

 

Hata hivyo anaripotiwa kufariki walipokutana nyumbani kwake huku watu wengine wattau wakiripotiwa kuwepo.Familia yake marehemu imepuzilia mbali taarifa kuwa alijitoa uhai.

 

 

 

 

 

 

 

 

March 8, 2023