Rais Mstaafu nchini Uhuru Kenyatta, adhuhuri ya leo aliwaongoza viongozi mbalimbali katika kumwomboleza aliyekuwa Waziri wa elimu nchini Prof. George Magoha, nyumbani kwake eneo la Lavington jijini Nairobi.

Rais mstaafu amemtaja mwendazake kama mtu aliyekuwa na moyo wa kusonga mbele na kufanya yale yaliyofaa, huku akiongoza katika mstari wa mbele kwenye maeneo yote aliyoteuliwa kuongoza.

Bw. Kenyatta amemwomboleza kama kiongozi aliyeleta mabadiliko chungu nzima katika idara ya mitihani ya kitaifa alipokuwa kiongozi wa KNEC na pia katika wizara ya elimu nchini. Rais Mstaafu aidha amesema kuwa hajutii chochote kwa kumteua kuwa Waziri wa elimu humu nchini.

Zaidi ya hayo, Kiongozi huyo wa zamani wa taifa ameonekana kuwapa mgongo viongozi wanaoeneza semi za kumdunisha akiwataka viongozi wenza akiwemo kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kutoyasikiliza wale wanayosema.

January 31, 2023