Maelfu ya wananchi wanaoishi katika nyumba za hali duni kwenye mitaa ya mabanda katika kaunti ya Nairobi wataanza kufurahia nyumba zenye hadhi iliyoinuliwa, na hii ni baada ya rais William Ruto kuwaongoza viongozi mbalimbali Pamoja na wananchi katika hafla ya kuweka msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika mtaa wa Shauri Moyo kaunti ya Nairobi alasiri ya leo.

Akizungumza katika hafla hiyo, rais Ruto aliweka peupe kuwa serikali yake imeweka mipango kabambe ya kuiondoa mitaa ya mabanda hasa katika kaunti ya Nairobi.

Rais ameeleza kuwa serikali imetenga ardhi ya ekari laki nne katika miji mbalimbali nchini, itakayotumika katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Naibu wa rais Rigathi Gachagua Pamoja na Gavana wa Kuanti ya Nairobi ambao walihudhuria hafla hii, wamesifia mradi huu wa ujenzi wa nyumba wakisema kuwa wakenya wengi watafaidika kuanzia kwa watakaojenga nyumba zenyewe hadi wapangaji katika nyumba hizi.

January 27, 2023