Margaret Nyakang'o

BY ISAYA BURUGU,13TH DEC,2023-Kesi ya jinai dhidi ya Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o imesimamishwa.Hii ni baada ya kesi ya Hakimu Alex Ithuku katika mahakama ya Mombasa kuambiwa kuwa kuna agizo la Mahakama ya Juu lililotolewa kusimamisha kufunguliwa kwake mashtaka.

Hakimu aliamuru kesi hiyo itajwe Mei 29, 2024.

Mahakama kuu ilitoa maagizo wiki jana baada ya kesi kuwasilishwa na Mbunge wa Mugirango Magharibi Stephen Mogaka kupitia kwa wakili Danstan Omari, kupinga mashtaka ya Nyakango.Katika karatasi za mahakama, Mogaka aliteta kuwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa Nyakang’o ni ukiukaji wa haki zake.

Nyakang’o, alikamatwa Mombasa mnamo Desemba 5, ambapo DPP aliidhinisha mashtaka mengi ya uhalifu dhidi yake na wengine 10.

 

 

 

 

 

 

December 13, 2023