BY ISAYA BURUGU,02,NOV 2022-Takribani yapata zaidi ya juma moja hivi baada ya mawaziri wapya chini ya utawala wa serikali ya Kenya Kwanza kuanza majukumu yao, Rais William Ruto ametangaza orodha ya makatibu wakuu 51.Majina hayo ni wale  waliochaguliwa kuhudumu katika nyadhifa tofauti za utumishi wa Umma.

Kwa mjibu wa taarifa kutoka kitengo cha habari cha rais ni kwamba,51 hao wamechaguliwa kutoka kwa orodha ya watu zaidi ya 500 ambao walihojiwa kuchukua nafasi hizo.

1. Makatibu Wakuu walioteuliwa ni pamoja na;

2. Julius Korir – Idara ya Masuala ya Baraza la Mawaziri

3. Teresia Mbaika Malokwe – Idara ya Ugatuzi

4. Esther Ngero – Idara ya Usimamizi wa Utendaji na Uwasilishaji

5. Aurelia Rono – Idara ya Masuala ya Bunge

6. Raymond Omollo – Idara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa

7. Caroline Nyawira Murage – Idara ya Magereza.

8. Amb. Julius Bitok – Idara ya Huduma za Wananchi

9. Dkt. Chris Kiptoo – Idara ya Hazina ya Kitaifa

10. James Muhati – Idara ya Mipango ya Kiuchumi

11. Patrick Mariro – Idara ya Ulinzi

12. Korir Sing’oei – Idara ya Masuala ya Kigeni.

13. Roseline Njogu – Idara ya Diaspora.

14. Amos Gathecha – Idara ya Utumishi wa Umma.

15. Veronica Mueni Nduva – Idara ya Jinsia na Usawa.

16. Joseph Mungai Mbugua – Idara ya Barabara.

17. Mohamed Dhagar – Idara ya Uchukuzi.

18. Nixon Korir – Idara ya  Ardhi na Mipango ya Miundomsingi.

19. Charles Hinga – Idara ya Ujenzi  na Maendeleo ya Miji

20. Joel Arumonyang – Idara ya Kazi za Umma

21. Edward Kisiangani – Idara ya Utangazaji na Mawasiliano ya Simu.

22. Eng. John Kipchumba Tanui – Idara ya ICT na Uchumi wa Dijitali

23. Eng. Peter Tum – Idara ya Huduma za Matibabu

24. Dkt. Joseph Mburu – Idara ya Viwango vya Afya na Usimamizi wa Kitaalamu.

25. Dkt. Belio Kipsang – Idara ya  Elimu ya Msingi

26. Esther Thaara Muhoria – Idara ya TVET

27. Beatrice Inyangala – Idara ya Elimu za Juu na Utafiti

28. Phillip Kello Harsama – Idara ya Maendeleo ya Mazao

29. Harry Kimutai – Idara ya Maendeleo ya Mifugo

30. Alfred K’Ombundo – Idara ya Biashara ya Jimbo

31. Abubakar Hassan – Idara ya Ukuzaji Uwekezaji

32. Juma Mukhwana – Idara ya Viwanda ya Jimbo

34. Patrick Kiburi Kilemi – Idara ya Vyama vya Ushirika

35. Susan Mangeni – Idara ya  Maendeleo ya MSMEs

36. Ismail Madey – Idara ya Masuala ya Vijana

37. Jonathan Mueke – Idara ya Michezo na Sanaa

November 2, 2022