BY ISAYA BURUGU,21ST FEB,2023-Rais William Ruto ametoa wito kwa mungano wa ulaya  kutamatisha makubaliano kadhaa ya kiuchumi kati yake na jumuia ya nchi za afrika mashariki  ili kuiwezesha Kenya kupanua uwezo wake wa uzaji bidhaa zake nje ya nchi.

Rais amesema hayoleo  alipofungua  warsha ya siku mbili ya kibiashara kati ya mungano wa ulaya na Kenya warsha ambayo imewaleta  Pamoja wafanyibiashara karibu mia tano  kutoka kenya na mungano wa ulaya.

Warsha ihiyo imeandaliwa na mungano wa ulaya kwa ushirikiano na mungano wa sekta ya kibinafsi nchini  na baraza la kibiashara la mungano wa ulaya.

Warsha hiyo inalenga  kufungua fursa za kibiashara kati ya Kenya na masoko yaliyoko ulaya.Rais Ruto  ameliambia baraza hilo la kibiashara la ulaya kuwa kenya inatoa fursa bora za uwekezaji kote katika kanda ya afrika mashariki hatua ambayo inaiweka nchi hii kwenye nafasi nzuri ya uwekezaji.Hivyo basi itakuwa bora Zaidi iwapo mikataba hiyo itamalizika kwa wakati.

 

 

 

February 21, 2023