Rais wa Angola João Lourenço alifanya mazungumzo ya simu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ili kujadili hali ya mzozo nchini Ukraine.Kupitia mtandao wa twitter,rais wa Ukraine alisema walijadili masuala ya ushirikiano ndani ya Umoja wa Mataifa.

Wawili hao pia walizungumzia kuhusu mashambulio ya makombora ya Urusi ya siku ya Jumatatu nchini Ukraine. Bw Zelensky amekuwa akizungumza na viongozi wa Afrika kutafuta uungwaji mkono wa kidiplomasia dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Angola ilikuwa ni miongoni mwa makumi ya nchi za Afrika ambazo zilijiondoa kwenye azimio la Umoja wa Mataifa mwezi Machi ambalo lililaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

 

October 11, 2022