BY Isaya Burugu,Oct 15,2022-Rais Wiliam Ruto  na naibu wake Rigathi Gachagua hivi leo waanaongoza hafla ya ufunguzi wa bwawa la Thiba kaunti ya Kirinyaga katika hatua inayotarajiwa kuwafaa pakubwa wakulima wa mpunga kutoka eneo hilo.

Kwa mjibu wa Daniel Nzwenzwe ambaye ni meneja wa mawasiliano katika mamlaka ya unyunyuziaji maji amesema ufunguzi wa bwawa hilo utapiga jeki pakubwa juhudi za kuwahakikishia wakulima maji ya kutosha mwaka mzima kuendeleza shughuli zao za ukulima

.Kwa upande wao wakaazi wamesifia hatua hiyo wanayosema sasa imetuliza matamanio wlaiokuwa nayo kwa muda mrefu ya kupata maji ili waweze kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Bwawa hilo limejengwa kwa dhamana ya shilingi bilioni 7 .8 na lilijengwa na serikali yar ais mstaafu Uhuru Kenyatta.

 

 

 

 

October 15, 2022