BY Isaya Burugu,Oct 15,2022-Viongozi wakidini katika kaunti ya Uasin Gishu  wanamtaka seneta wakaunti hiyo Jackson Mandago kujiepusha na kutoa matamshi yanaweza leta migawinyiko kati ya wanaoishi katika kaunti hiyo.

Viongozi hao badala yake wanamtaka Mandago kufanya kazi aliyopewa.Wakiongozwa na askofu Paul Gathuo,

wamesema kuwa siasa ziliisha baada ya uchaguzi kumalizika,na hakuna haja aya Mandago ambaye awali alikuwa gavana kuendelea kukshafu watu wa jamii zingine katika kaunti hiyo ambao wlaikuwa na msiammo tofauti wakisiasa kwnai ilikuwa ni haki yao yakikatiba kuunga mkono upande ambao wanataka.

Wakizungumza mjini Eldoret viongozi hao pia wamemtaka gavana Jonathan Bii kuwa katika mstari wa mbele kuunganisha watu wanaoishi katika kaunti hiyo.

October 15, 2022