Rais William Ruto amefungua rasmi afisi mpya za UDA eneo la Kati katika mji wa Nyeri.

Rais Ruto aliwashukuru wakazi wa eneo hilo kwa kuunga mkono UDA na kuongeza kuwa watafanya uchaguzi mwezi Desemba ili kuwachagua viongozi wa chama.Alisema hatua hiyo itaimarisha na kupanua chama hicho tawala hadi ngazi ya kitaifa ili kuunganisha nchi.

Aidha kwa mara nyingine mkuu wa nchi amewahimiza wakaazi hao kutojihusisha na masuala fujo yanayochangia uharibifu wa mali.

Ruto aliandamana na Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, mwenyekiti wa UDA Cecily Mbarire, katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala na Mbunge wa Kiharu Ndidi Nyoro miongoni mwa wengine.

Share the love
September 9, 2023