Naibu mkuu wa majeshi ya Kenya Luteni jenerali Jonah Mwangi amesema kuwa zoezi la usajili wa makurutu lililokamilika jana kote nchini lilikuwa huru na wa haki na lilifanikiwa.

Luteni Mwangi alieleza kuwa kufanikiwa huko kulifuatia ushirikiano kati ya asasi za usalama,idara za kupambana na ufisadi nchini pamoja na wananchi.

Vilevile Luteni Mwangi aliwasifu wale wote walioshiriki katika zoezi hilo akisema waliofaulu katika nyadhifa za cadets watajulishwa kupitia Tovuti rasmi ya Wizara ya Ulinzi au kupitia vyombo vya habari kati ya tarehe 17 na 24 Septemba 2023.

September 9, 2023