Rais William Ruto amejitokeza kumtetea Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman baada ya kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kumtishia kufuatia matamshi yake kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Akizungumza jijini Nairobi, Rais Ruto alimsuta Kiongozi huyo wa Azimio kwa kile alichokitaja kuwa kutoa matamshi ya ovyo dhidi ya balozi wa Marekani.

Alikariri kuwa Marekani ndiyo soko kubwa zaidi la kigeni kwa Kenya na kwamba kutoa maoni kama hayo ni sawa na kuharibu uchumi wa nchi.

Odinga, katika hotuba yake siku ya Alhamisi wakati wa Kongamano la Ugatuzi, alimtaja Whitman kama ‘tapeli’, kwa kudai kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2022 ulikuwa wa kuaminika zaidi katika historia ya nchi.

August 18, 2023