Rais William Ruto amesisitiza kwa mara nyingine kujitolea kwa taifa la Kenya katika kulipiga jeki taifa la DRC Congo na kulisaidia ili kukabiliana na changamoto nyingi zinazolikumba taifa hilo.

Rais Ruto aliyasema haya katika hotuba yake nchini DRC alikowasili ili kufanya mashauriano na kueneza ujumbe wa amani ili kusitisha mapigano. Ziara ya rais Ruto nchini Congo imefanyika baada ya ziara ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta ambaye amepewa jukumu la kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Kongo kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa Congo Felix Tshisekedi na Rais Ruto pia wameandaa majadiliano juu ya mahusiano ya biashara baina ya mataifa haya mawili, kuhusu ushirikiano wa kikanda na usalama katika eneo la mashariki mwa Congo.

November 21, 2022