Rais William Ruto amesisitiza msimamo wake kwamba hatakubali kugawana nyadhifa za uongozi na upinzani kwa njia yoyote ile.

Akiwahutubia wananchi katika eneo la Githurai kaunti ya Kiambu baada ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo, Rais amesema kwamba hatakubali kuyumbishwa na vitiso vya upinzani, na badala yake ameahidi kuwa serikali ya Kenya Kwanza itaendelea kutekeleza mipango yake kwa wakenya kama ilivyoahidi kwenye manifesto.

Semi za rais aidha zimejiri huku Vikosi vya mazungumzo ya mapatano kati ya Serikali na Upinzani vikijiandaa kuanza mazungumzo yao.

Share the love
August 5, 2023