Kazi mtaani imeisha

Rais William Ruto amevunja mpango wa kazi mtaani ambao ulikua ukitoa nafasi za kazi za kusafisha kwa vijana, na badala yake kusema kuwa vijana sasa watahusishwa katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Akizungumza katika mtaa wa Soweto mashariki eneobunge la kibera ambapo aliongoza hafla ya kuzindua mpangowa ujenzi wa nyumba za bei nafuu, Rais Ruto amesema kuwa vijana watapata nafasi za ajira wakati wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu na kuwawezesha kupata kipato chao cha kila siku badala ya kurejea katika mpango wa kazi Mtaani.

Katika mpango huu, Serikali inapani akujenga angalau nyumba laki mbili kila mwaka jambo ambalo litalisaidia taifa kuafikia ajenda yake ya makaazi ya beni nafuu kwa wananchi wa kipato cha chini. Ruto ameahidi kuwa mpango huo utawahusisha vijana kutoka wadi zote ambapo ujenzi huu utakua unatekelezwa.

YouTube player

Iwapo mpango huu utafanikiwa, Rais ameweka wazi kuwa kila mpangaji atalipa shilingi 2,500 kwa mwezi na baada ya miaka ishirini, wapangaji hao watakuwa wamiliki wa nyumba hizo.

October 25, 2022