Inspekta jenerali wa polisi mteule Japheth Koome anatarajiwa kufika mbele ya kamati za bunge la seneti na lile la kitaifa kwa zoezi la kupigwa msasa kabla ya kuidhinishwa kutwaa wadhfa huo. Koome atafika mbele ya kamati hizo tarehe 8 mwezi ujao. Kulingana na karani wa bunge la kitaifa Serah Kioko, Bw. Koome atatakiwa kuwasilisha kitambulisho chake rasmi na vyeti vya masomo na kitaaluma. Koome aliteuliwa kwenye wadhifa huo na Rais William Ruto mnamo Septemba 27, baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi anayeondoka Hillary Mutyambai, kuamua kuendelea na likizo ya mwisho kabla ya kukamilika kwa muda wake afisini kutokana na matatizo ya kiafya.Bw. Koome, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi, ndiye Kamanda wa sasa wa Chuo cha Kitaifa cha Huduma ya Polisi, Kiganjo.

October 25, 2022