Egerton University Strike

Mahakama ya Ajira mjini Nakuru imeamuru kusitishwa mara moja kwa mgomo wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Egerton ili kutoa mwanya kwa mazungumzo kati ya pande husika.

Katika uamuzi wake siku ya Jumanne 25.10.2022, Jaji Hellen Wasilwa ameagiza usimamizi wa chuo hicho pamoja na viongozi wa muungano wa kutetea maslahi ya wafanyikazi wa vyuo vikuu UASU, kuandaa mazungumzo na kutatua mizozo yao ili kuruhusu shughuli za masomo kurejelewa, huku mahakama ikitarajiwa kutoa mwongozo Zaidi kuhusiana na mzozo huo tarehe mosi mwezi Disemba.

Wahadhiri wa chuo cha Egerton wako katika juma la pili la mgomo, wakipinga kile walichokitaja kama kupunguzwa kwa mishahara yao kwa asilimia 43 kuanzia mwaka wa 2020.

October 25, 2022