Rais William Ruto amewasili katika taifa la Korea kusini kwa ziara rasmi katika taifa hilo ambapo anatarajiw akuandaa mashauriano na rais Yoon Suk Yeol.

Rais Ruto aliwasili katika taifa la Kora Kusini adhuhuri ya leo Jumanne 22.11.2022, na anatarajiwa kuendeleza mashauriano na wakuu wa sekta mbalimbali katika taifa hilo, sawa na kuhudhuria kongamano la uwekezaji ili kuliuza taifa kama eneo nzuri la uwekezaji.

Idara ya mawasiliano ya ikulu imeweka wazi kuwa ziara hii ya rais itafungua njia kwa wawekezaji kutoka katika taifa hilo lenye ukwasi wa teknolojia. Vilevile rais alipata fursa ya kutagusana na hata kuwahutubia wakenya wanaoishi katika taifa hilo.

November 22, 2022