Rais William Ruto amesema serikali itapanua uhusiano wa kiuchumi na Korea Kusini ili kubuni nafasi za biashara na ajira kwa wakenya. Akizungumza wakati wa mkutano nchini Korea Kusini, Rais Ruto alisema Kenya itashirikiana na Serikali ya Korea Kusini kufungua fursa katika teknolojia, biashara, uwekezaji na shughuli za baharini.

Aliongeza kuwa Kenya itatumia ujuzi wa wakenya ambao ni mojawapo ya bora duniani.Mazungumzo hayo kati ya Kenya na Korea Kusini pia yanalenga kupata masoko ya bidhaa za Kenya nchini humo.

Rais Ruto vilevile alisema Kenya itashirikiana kwa karibu na Serikali ya Korea kuimarisha nishati safi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa uapnde wake spika Kim Jin Pyo aliahidi kuunga mkono azma ya Kenya ya kuongeza mauzo ya kilimo nchini Korea Kusini na kupata nafasi za kazi kwa Wakenya.

November 23, 2022