Rais William Ruto ameusuta muungano wa Azimio unaoongozwa na Raila Odinga kwa kuandaa msururu wa maandamano nchini kote ili kupinga Sheria ya Fedha ya 2023 na gharama ya juu ya maisha.

Akizungumza katika kaunti ya vihiga, Rais Ruto amesema Wakenya tayari walimpigia kura kama kiongozi wanayempendelea katika uchaguzi wa 2022, lakini ikiwa upinzani bado unataka kutoa msukumo wa kuiongoza nchi, unaweza kusubiri 2027.

Kuhusu suala la sheria ya fedha ya mwaka 2023, Ruto ameutaka upinzani kukoma kushinikiza kubatilishwa kwa Sheria hiyo akisisitiza kuwa itasaidia kutengeneza fursa za ajira kwa vijana.

July 22, 2023