Papa Francis amemteua askofu Paul Kariuki Njiru wa Jimbo Katoliki la Embu kama askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Wote. Baba Mtakatifu, Papa Francisko ameanzisha Jimbo jipya la Wote, na kulitenganisha na Jimbo kuu la Machakos.

Habari za kuanzishwa kwa jimbo la Wote na kuteuliwa kwa Askofu Kariuki zilichapishwa rasmi katika gazeti rasmi la Roma mnamo tarehe 22 Julai 2023 saa 12:00 mchana kwa saa za Roma na saa 1:00 mchana kwa saa za Kenya.

Mwakilishi wa papa nchini Kenya na Sudan Kusini, Askofu Mkuu Bert van Megen, pia alituma mawasiliano rasmi kwa Baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki KCCB.

Share the love
July 22, 2023