Rais William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua wamepata alama ya D katika utendakazi wao. Hii ni kulingana na kura ya maoni ya iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya InfoTrak.

Utafiti huo uliotolewa leo pia imeonyesha kuwa waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ndiye waziri anayefanya  vyema ambapo amepata asilimia 60, akifuatiwa na mwenzake wa Michezo Ababu Namwamba ambaye amepata asilimia 51.

Mtafiti mkuu wa InfoTrak Johvine Wanyingo aliongeza kuwa mawaziri Soipan Tuya (Misitu), Aden Duale (Ulinzi) na Eliud Owalo (ICT) walipata asilimia 48 huku waziri wa Kilimo Mithika Linturi akiibuka wa mwisho kwa kupata asilimia 39 baada ya Waziri wa Nishati Davis Chirchir.

June 10, 2024