Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewapongeza waandishi wa habari kwa kutangaza taarifa za Amani na kudumishwa kwa usalama kote nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua awamu ya nne ya ruwaza ya mwaka 2030 katika kaunti ya Marsabit, Kindiki ameeleza kuwa taarifa hizo zimesaidia katika kupunguza uhasama na uchochezi baina ya jamii mbalimbali humu nchini.

Kindiki aidha amewarai wanahabari kutotumia vibaya uhuru wao wa uandishi wa habari.

June 10, 2024