Mbunge Mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Narok kwenye bunge la Kitaifa Rebecca Tonkei amempongeza mkurungenzi wa elimu katika kaunti ya Narok Jane Mutai kwa kuhakikisha kwamba haki na uwazi zilizingatiwa wakati wa zoezi lililopta hivi majuzi la uajiri wa walimu.

Akizungumza katika shule ya upili ya Olkiriainie kwenye kaunti ndogo ya Narok kusini alikohudhuria hafla ya kutoa shukrani kwa matokeo bora ya KCSE shuleni humo mwaka uliopita, Bi. Tonkei alisema kwamba walimu ambao walihitimu kutoka kaunti ya Narok ndio walipewa kipau mbele katika zoezi hilo la uajiri.

Mbunge huyo kadhalika, amedai kwamba hapo awali walimu kutoka kaunti husika walikuwa wakitengwa licha ya wao kuhitimu saw ana wenzao kutoka pembe tofauti za taifa.

March 3, 2023