BY ISAYA BURUGU,4TH MARCH,2023-Mtu mmoja  amefariki baada ya kugongwa na gari  eneo la  Kiangwaci  kwenye barabara kuu ya  Sagana-Karatina  katika eneo bunge la Ndia,kaunti ya  Kirinyaga. Wenyeji wameawambia wandishi Habari kuwa  marehemu alikuwa ndio manzo anajiandaa kupanda gari  wakati alipogongwa na gari.

Wakati huo huo wenyeji wamelalama kuhusu visa vinavyozidi kuongezeka vya ajali za barabarani  katika barabara hiyo yenye shughuli nyini.

Wamemtaka mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kukarabati barabara hiyo kuweka mabango yanayoonya watumizi wa barabara hiyo  ili kuzuia visa kama hivyo .

Mwili wa Mwenda zake umepelekwa katika hifadhi ya maiti  iliko karibu huku gari lenyewe likipelekwa kiuo cha polisi cha Sagana.

 

March 4, 2023