Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji amebadili msimamo wake na kuondoa ombi la kutaka kusitishwa kwa kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa gavana wa Samburu Moses Lenolkulal katika mahakama ya Milimani.

Lenolkulal alikabiliwa na kesi ya ufujaji wa kima cha shilingi milioni 80.7 mnamo mwaka wa 2019.Msimamizi mkuu wa mashtaka Alexander Muteti amesema kuwa yuko tayari kuendelea na kesi hiyo hadi tamati.

Uamuzi wa Haji umejiri siku moja baada ya chama cha mawakili nchini LSK kumpaa makataa ya siku tatu ili aweze kutoa sababu dhabiti kuhusiana na hatua yake ya kutupilia mbali kesi za ufisadi dhidi ya maafisa wakuu serikalini.

Siku mbili zilizopita afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma iliondoa kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa mbunge wa malindi Aisha Jumwa.Jumwa alikuwa akikabiliwa na kesi ya ufisadi ya shilingi milioni kumi na tisa,pesa anazodaiwa kuziiba kutoka kwa hazina ya maendeleo ya maeneobunge.

October 14, 2022