Serikali ya kaunti ya Narok itashirikiana na serikali ya kitaifa ili kujenga majumba ya kisasa. Hii ni kauli yake mhandisi B.M. Njenga.

Akizungumza mjini Narok wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Bw.Njenga aliyeandamana na gavana wa kaunti hii Patrick Ntutu amesema ushirikiano baina ya serikali hizo mbili utaimarisha hadhi ya mji wa Narok haswa masoko.

Kauli ya Njenga imeungwa mkono na gavana Ntutu ambaye amehaidi kuboresha miundo misingi yakiwemo masoko ya Muthurwa ,Uhuru, Ololulunga pamoja  na  Ntulele

Naye kwa upande wake kamishana wa kaunti hii Isaac Masinde amesema kuwa wanapania kuboresha mazingira ya masoko humu mjini ili kubuni nafasi kwa wafanyabiashara zaidi.

January 19, 2023