BY ISAYA BURUGU,7TH MARCH,2023-Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i  angali anahojiwa  katika makao makuu ya DCI.Hi ni baada yake kuwasili katika makao hayo saa mbili unusu za  asubuhi.Mawakili wa Matyang’i walikuwa wamesema kwamba mteja wao angewasili katika makao makuu ya DCI mwendo wa saa mbili, saa moja kabla ya muda aliyoelekezwa.

Wakili wake Danstan Omari alisema kwamba alimwandikia afisa wa mwaliko kumjulisha kuhusu mabadiliko hayo. Richard Onyonka ni seneta wa Kisii

.Matiang’i anahojiwa kuhusiana na madai ya polisi kuvamia nyumba yake huko Karen usiku wa Februari 8.

Polisi na idara zote za usalama walikanusha kuhusika na uvamizi huo wakidai kuwa uzushi.

Omari alisema waziri huyo wa zamani yuko tayari kurekodi taarifa yake kuhusu uvamizi huo akisema hangeweza kufanya hivyo hapo awali kwa vile wito uliotolewa Februari 23 hawakupewa kamwe.

 

 

 

 

March 7, 2023