Serikali imeahirisha uzinduzi wa Maisha Namba na kitambulisho cha kidijitali ambacho kingezinduliwa na Rais William Ruto mnamo Jumatatu, Oktoba 2, 2023.

Katika taarifa iliyotolewa hii leo na katibu wa idara ya Uhamiaji Julius Bitok, uzinduzi huo uliokuwa ufanyike katika uwanja wa Riadha, Kaunti ya Nakuru, umesitishwa kutokana na sababu zisizoweza kuepukika.

Prof. Bitok alisema tarehe mpya ya kuzinduliwa kwa Maisha Namba itatangazwa kwa wakati ufaao. Katibu huyo hata hivyo alisisitiza kwamba ushiriki wa umma unaoendelea nchini kote na mijadala ya washikadau kuhusu Maisha Namba utaendelea kama ilivyopangwa.

September 29, 2023