Serikali itawapa maafisa wa usalama vifaa vya kisasa vya kuwalinda dhidi ya wahalifu waliojihami na kuwawezesha kuwalinda Wakenya na mali zao.Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki.

Akizungumza Jumatatu katika Kaunti ya Wajir wakati wa kutathmini utendakazi wa maafisa wa usalama katika Kaunti Ndogo ya Kotulo huko Tarbaj, Kindiki alipongeza maafisa wa usalama kutoka mashirika yote kwa kufanya kazi kwa bidii ili kupambana na wahalifu katika eneo la Kaskazini Mashariki.

Prof Kindiki wakati uo huo aliwataka raia wote kufanya kazi kwa ukaribu na maafisa wa usalama na kupinga majaribio ya vikundi vya kigaidi kuwaingiza vijana katika vikundi hivyo.

September 18, 2023