BY ISAYA BURUGU,05,NOV 2022-Waziri wa uchukuzi  Kipchumba Murkomen ametaja mgomo wawafanyikazi wa shirika la ndege nchini Kenya Aiways  kuwa kinyume cha sheria na usiohalali.Haya yanajiri  baada ya sehemu ya  marubani wa shirika hilo   na wale wa mungano wa marubani nchini KALPA  kuanza mgomo wao rasmi hivi leo asubuhi  na kusambaratisha  shughuli za usafiri za shirika hilo.

Mkurugenzi mkuu wa Kenya Airways Alan Kivaluka amewapa marubani hao muda was aa 24 wawe wamerejea kazini au wachukuliwe hatua za kisheria.Afisa huyo anasema kuwa wamekuwa mkutanoni kwa Zaidi ya saa tano na marubani hao wakilenga kupata suluhu na juhudi hizo haziwezi kuchukuliwa kimzaha.

Hivi leo Waziri Murkomen aliyeandamana na mkurugenzi mkuu wa KQ amesema usimamizi wa shirika hilo umewasilikiliza marubani hao na maswala wanayoibua na liko tayari kufanya mazungumzo yatakayopelekea suluhu kupatikana.Marubani hao wanaitisha nyongesa ya mshahara na marupurupu sawa   na kuboreshwa kwa mazingira ya utenda kazi.

Wakati hayo yakijiri abiria waliokuwa na hasira wamewakashfu Waziri Murkomen  na mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege nchini Kenya Airways kwa kutoweka mikakati mwafaka ya awali ili kuwaondolea dhiki.Abiria hao waliozungumza katika uwanja wa ndege wa JKIA   wamesema usimamizi wa shirika hilo na serikali walikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wateja waliokuwa wamepanga safari na hata kulipia nauli zao za ndege kuelekea katika sehemu mbali mbali za ulimwengu hawatatiziki na mgomo huo.

 

 

 

 

November 5, 2022