BY ISAYA BURUGU,05,NOV 2022-Serikali ya kitaifa imeanzisha zoezi la usambazaji wa chakula kuzisaidia familia zilizoadhirika na uhaba  wachakula kufuatia kiangazi kinachoshuhudiwa katika sehemu mbali mbali nchini.Zoezi hilo linalenga kaunti 12 kote nchini zilizoadhirika vibaya.Naibu rais Rigathi Gachagua,amaezindua zoezi hilo la usamabzaji wa chakula na unuzi wa mifugo katika eneo la Ilbisili kaunti ya Kajiado.

Naibu rais aliyendamana na gavana wa kaunti ya Kajiado Joseph Ole Lenku amazindua zoezi la usafirishaji wa chakula cha mifugo na wanazindua zoezi lingine  eneo la Nakalale kaunti ya Turkana na baadaye Baragoi huko Samburu.

Rais Wiliam Ruto anaratajiwa kuongoza zoezi la usambazaji chakula eneo la Nakalale huko Turkana na Kisha Baragoi kaunti ya Samburu.

Naye mkewe rais Racheal Ruto na mkewe naibu rais Bi Dorcas Rigathi wanasambaza kwa Pamoja chakula katika maeneo ya mabanda jijini Nairobi ambapo watazuru mitaa ya mukuru kayaba embakasi na kahawa soweto huko Kasarani kutoa msaada huo.

 

 

 

November 5, 2022