BY ISAYA BURUGU,17TH SEPT,2022-Mgombea urais wa Roots Party katika kinyang’anyiro cha Agosti 9  George Wajackoyah amemaliza kukarabati nyumba ya marehemu babake.

Siku ya Ijumaa Wajackoyah alionyesha nyumba ya zamani ya marehemu Tito Jakoya Odhiambo na ile mpya iliyopanuliwa na kuboreshwa kwa vioo.

Mwanasiasa huyo ambaye aliibuka wa tatu katika kinyang’anyiro cha urais alisema hatua hiyo ilifuatia maridhiano yake na babake.

Pia alionyesha kaburi la marehemu baba yake lililo nje kidogo ya nyumba hiyo ambalo pia aliifanyia ukarabati kwa marumaru.Marehemu Jakoya alifariki mnamo Desemba 21, 2021 akiwa na umri wa miaka 86.Hii ilikuwa miezi michache tu kabla ya Wajackoyah kutangaza azma yake kuwania urais wa Kenya katika uchaguzi wa mwaka huu.

Wakili huyo aliidhinishwa kuwania kiti hicho cha juu zaidi mapema mwezi Juni baada ya kutimiza matakwa ya IEBC.Wajackoyah aliibuka wa tatu katika kinyang’anyiro hicho ambacho kilishindwa na mgombea wa UDA William Ruto.

 

September 17, 2022