BY ISAYA BURUGU,17TH SEPT 2022-Huku shule zikitarajiwa kufungwa kwa likizo fupi kabla ya kufunguliwa kwa muhula wa tatu na wa mwisho mwaka huu,wazazi wametakiwa kuwapa ushauri nasaha Watoto wao.

Mwenyekiti wa chama cha kutetea maslahi ya wazazi kaunti ya Tranzoia ,Welington Waliaula,amedokeza kuwa wazazi wengi wameshindwa kutoa ushauri huo kwa Watoto wao hali ambayo imechangia katika kuongeza utovu wa nidhamu miongoni mwao.

Pia ametoa wito kwa wazazi kuwa macho ya wanafuzni wanapokuwa nyumbani na kuwalinda dhidi ya visa vya dhulma vinavyowapata Watoto.

September 17, 2022