By Isaya Burugu,Oct 8,2022-Aliyekuwa mbunge wa Ainabkoi William Chepkut ameaga dunia.Kwa mjibu wa familia yake iliyodhibitisha kifo hicho,Chepkut amefariki leo asubuhi.

Mbunge huyo wa zamani anasemekana kuzirai akiwa nyumbani kwake  na kupelekwa katika hospitali ya Mediheal iliyoko eneo la parklands ambapo madakitari wametangaza kuwa ameaga dunia.

Inasemekana Chepkut amefariki kutokana na kuganda kwa  damu na shinikizo la damu.Mwaka uliyopita Chepkut alikuwa amelazwa hospitalini na kusalia huko kwa muda wa miezi miwili  baada ya kupata ajali akiwa hotelini ambapo aliteleza na kuangauka kabla ya kubingiria mara kadhaa.

Pia alikuwa  amepata  ajali ambayo ilimlazimu kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Chepkut alikuwa mbunge wa Ainabkoi katika ya mwaka 2017 na 2022.

Alijaribu kutetea kiti chake kwenye uchaguzi wa Mwezi Agosti mwaka huu kama mgombea huru lakini akapoteza kwa Samuel Chepkonga wa UDA.

 

October 8, 2022