Waziri wa usalama wa Ndani Dkt. Fred Matiang’i ametangaza kuwa siku ya Jumatatu, Oktoba 10, 2022 kuwa likizo ya umma kuwaruhusu wananchi kuiadhimisha siku ya Utamaduni humu nchini. Waziri Matiang’i, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mapema leo, alisema siku hiyo imetengwa kusherehekea tamaduni mbalimbali nchini, na hivyo kuwataka Wakenya kusherehekea tofauti kati ya mila mbalimbali pamoja na kujifunza kukumbatia utofauti wa mila na tamaduni hizi.

October 7, 2022