Waziri mteule wa masuala ya Jinsia Aisha Jumwa amepata afueni baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma kuondoa kesi ya ufisadi dhidi yake.

Jumwa alikuwa akikabiliwa na kesi ya ufisadi ya shilingi milioni kumi na tisa,pesa anazodaiwa kuziiba kutoka kwa hazina ya maendeleo ya maeneobunge.

Kupitia afisa wa DPP Alex Akula, upande wa mashtaka umemomba hakimu mkuu Martha Mutuku kuondoa mashtaka hayo ila kesi itasalia kwa washtakiwa wenza wanne ambao sasa watajibu mashtaka upya.

Aidha Jumwa bado anakumbwa na mashtaka ya mauaji huku akitarajiwa kuhojiwa na bunge kabla ya kuapishwa rasmi kuwa waziri.

October 12, 2022