Mpango wa serikali wa kuagiza mahindi ya Kisaki au GMO umepigwa breki baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kusitisha uagizaji wa vyakula hivi.

Agizo hili limetolewa kusitisha uagizaji wa vyakula hivi hadi itakapoamuliwa kesi iliyowasilishwa mahakamani na muungano wa wakulima wadogo wa Kenya Peasants League ukipinga amri ya serikali ya luagiza chakua hiki.

Jaji wa mahakama kuu Mugure Thande amesitisha mpango huu na kuitaka serikali kutosambaza chakula chochote cha GMO kwa wakenya humu nchini. Kesi hii inatarajiwa kusikilizwa tarehe 15 mwezi kesho.

November 28, 2022