BY ISAYA BURUGU,27TH FEB,2023- Askofu mkuu wa jimbo kuu la Nyeri Anthony Muheria amesema kuwa kama kanisa katoliki hawakubaliani kamwe na maamuzi ya mahakama ya juu kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja.Askofu Muheria amedokeza kuwa ingawaje kuna haja ya kumpenda kila mmoja hawawezi kubali matendo ya mapenzi ya jinsia moja.

 Wakati huo huo askofu wa kanisa la Community Christian Church  ameongeza sauti yake katika swala la kuruhusu mabasha na mashoga kubuni muungano.Askofu Sayalel  ameSHUTUMU UAMUZI HUO ANAosema unakwenda kinyume na maadili yakijamii na watu wa Kenya.Uamuzi huo vilevile umepingwa na vingozi wa kisiasa wa hivi punde akiwa ni spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula ambaye amesema kuwa uamuzi huo utavunja kanuni za kitamaduni katika taifa la kenya.

Wetangula alioengeza kuwa Kenya ni taifa linalomcha Mungu na hivyo basi uamuzi kama huo hauwezi ukatekelezwa humu nchini.

Itakumbukwa kwamba siku ya  Ijumaa, Mahakama ya Juu ilisema kuwa uamuzi wa kuwanyima wanachama wa LGBTQ haki yao ya kujiandikisha kama NGO, licha ya ushoga kuwa haramu katika taifa, ulikuwa wa kibaguzi.

February 27, 2023