Zoezi la kuhesabu kura nchini Negeria linaendelea ingawa mashambulizi kadhaa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo yalichelewesha zoezi hilo.

Matokeo kutoka vituo mbalimbali vya kupiga kura kote nchini humo yapo katika mchakato wa kujumuishwa, baada ya ucheleweshwaji mkubwa.

Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa mashambulizi hasa katika mji mkuu wa kibiashara Lagos.

Takriban wapiga kura milioni 87.2 walikuwa na vigezo vya kupiga kura ya kumchagua mrithi wa rais Muhammadu Buhari aliyehudumu kwa mihula miwili, huku changamoto ya maisha bora,vurugu za makundi ya uasi pamoja na mzozo wa noti vikiwa miongoni mwa vibarua vigumu kwa rais mpya atakayeingia madarakani.

 

February 27, 2023