BY ISAYA BURUGU,27TH FEB,2023-Wanafunzi wa shule ya upili ya Ololulunga Narok kusini wamegoma na kufanya mandamano hadi soko la Ololulunga kufuatia kile walichokitaja kuwa  uongozi mbya wa shule hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari naibu kamishana wa Narok kusini Felix Kisalu amesema hajabainika nini kilasababisha Wanafunzi hao kuondoka shuleni.Kisalu amesema mafisa wa usalama wameingilia kati kwa haraka na hakuna uharibifu ambao umefanyika katika shule hiyo.

Kisalu aidha ameongeza kuwa hakuna taharuki miogoni mwao akisema ofisi yake imejaribu kuingilia kati kutuliza hali huku wanafunzi wapatao 200 wakikubali kurudi shuleni kati ya 1000 huku wengine wakiamua  kwenda nyumbani.Kamati ya usalama na usimamizi wa shule hiyo inatarajiwa kufanya mkutano leo kutathmini mstakabali wa shule hiyo hiyo.

 

 

 

February 27, 2023