Maandamano Upinzani

Muungano wa upinzani nchini umewasilisha kesi mahakamani, kuishtaki serikali na kuitisha fidia kwa watu 75 wanaodaiwa kuuwawa na maafisa wa polisi katika maandamano ya kupinga ongezeko la gharama ya maisha nchini.

Wakili wa muungano huo, Paul Mwangi, amesema kwamba viongozi wa idara za polisi wanafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Amesema kwamba maafisa hao walitoa amri ya kupigwa risasi kwa wananchi waliokuwa wakishiriki katika zoezi lililokubalika kisheria.

Kando na kudai fidia kwa ajili ya familia za waliopoteza maisha, muungano wa upinzani pia unaitaka mahakama kutoa agizo la kuchunguzwa kwa idara za usalama ili kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kuwadhulumu raia waliokuwa wakidai haki yao.

 

 

Share the love
October 13, 2023