BY ISAYA BURUGU,17TH SEPT,2022-Mazishi ya aliyekuwa mwanzilishi wa baraza la wazee la jamii ya wamasai Marehemu John Ole Maitai ambayo yalikuwa yafanyike hivi leo yameweza kuairishwa hadi Alahamisi ijayo.

Haya ni kwa mjibu wa familia ya Mwenda zake ikiongozwa na Emanuel Ole Maitai ambaye ni kifungua mimba wa marehemu na pia msemaji wa familia ambaye amesema wamelaziika kuiarisha mazishi hayo kama familia kwa sababu ambazo hawangeweza kuziepuka.

Pia amesema marehemu ambaye alikuwa azikwe Gilgil kaunti ya Nakuru sasa atazikwa eneo la Oloropili kaunti hii ya Narok.

September 17, 2022